WANAWAKE NISIKILIZENI MWALIMU WENU...MI SIO MWALIMU KIPOFU.
1.
Anakupigia simu mara kwa mara na kukuuliza siku yako imeendaje.
Anafanya hivi kirafiki na kwa upendo, haigizi. Anakupenda kweli.
2.
Anakutembelea mara kwa mara, anakuwa karibu na wewe kipindi unaumwa, hii
inamaanisha kwamba yupo tayari kukuvumilia katika shida na raha. Mpende
mwanaume huyu.
3. Anawapenda ndugu zako kama ndugu zake. Anaongea nao vizuri na kusaidiana mambo ya hapa na pale. Mtizame kwa jicho la tatu huyu mwanaume!
4. Anaongea na wewe kwa adabu na kwa upole, anakukosoa bila wasiwasi
kama kuna mambo unaenenda visivyo. Anakuelekeza njia zilizonyoka..sio wa
kumuacha huyu!
5. Hakulazimishi kufanya mapenzi. Anakupenda sana
kiasi kwamba hawezi kukulazimisha jambo ambalo hauko na hiari nalo. Yupo
karibu na wewe wakati wote na sio tu anapokutaka kimapenzi, huyu ni
bonge la bwana.
6. Anakusaidia fedha pale unapokua umekwama kabisa,
yuko na jukumu la kukusaidia kiuchumi. Anapenda kukupa kile ambacho
amejaaliwa nacho. Hana mkono wa birika, Huyu anakupenda!
7.
Anazungumzia future yake na wewe, mipango ya baadae pamoja na wewe, huyu
anayo dhamira ya dhati kutoka moyoni mwake ya kukufanya uwe mkewe.
Hizi ni moja ya dalili kwamba mwanaume wako anakupenda na anataka
atengeneze future pamoja na wewe. Usikate tamaa juu ya mwanaume wa aina
hii.
Hao wenye sixpack sijui eight pack, wabeba vyuma, wavaa
milegezo, wanyonya midomo na mahandsome wavaa hereni, masupa staa,
watoto wa vigogo, hawatakusaidia lolote, utabaki ukiumizwa tu moyo wako.
Kabla hujajipendekeza kwa wanaume wa aina hiyo, jiulize wanawake
wanzako wangapi wameshajipendekeza kwa sababu ya hzo pesa zake, hivyo na
wewe unajiongeza kwenye foleni!
Mvumilie mwanaume wako, anazo ndoto
njema, mapenzi ya kweli ni vigumu sana kuyapata. Ila pesa na mali ni
rahisi sana kuzipata kama utajibidiisha.
Usipende mitelemko, mitelemko mingine ni njia ziletazo mauti! - Ukishikwa shikamana, ukipendwa, pendeka!
No comments:
Post a Comment