Tuesday, 16 August 2016
WAZIRI AJIUZULU KWA ULEVI NCHINI SWEDEN
Waziri wa kwanza mwenye umri mdogo Sweden, aliyeingia nchini humo kama mkimbizi kutoka Bosnia, ametangaza kujiuzulu baada ya kukamatwa akiendesha gari akiwa amelewa.
Aida Hadzialic, mwenye umri wa miaka 29 ambaye ni waziri wa elimu ya shule ya sekondari na elimu ya watu wazima, alifichua kuwa alikuwa amesimamishwa na polisi katika mji wa kusini wa Malmo akiwa amelewa. Alisema vipimo vilivyochukuliwa na polisi vilionyesha alikuwa na gramu 0.2 ya pombe katika kila lita moja ya damu, kiwango ambacho kinachukuliwa kuwa kosa nchini humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment