Polisi Mkoa wa Shinyanga inafanya uchunguzi wa madai ya askari wake kula
chipsi na kukataa kulipa kisha kuanzisha fujo baada ya kudaiwa fedha.
Askari hao zaidi ya watatu wanadaiwa kuagiza watengenezewe chipsi na mayai na kukataa kulipa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Muliro Jumanne amesema tukio hilo
lilitokea Agosti 13 eneo la Mshikamano Kata ya Ngokolo Manispaa ya
Shinyanga saa nne usiku.
No comments:
Post a Comment