Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. Mongella atoa kauli hii kwa wanafirsa leo.
“Ukizungumzia fursa
za kiuchumi na kibiashara mkoani Mwanza, lazima utaje sekta za kilimo,
uvuvi, ufugaji na madini. Ndizo uti wa mgongo wa mkoa wa huu,” anasema
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.
Anasema Serikali
inakusudia kuwawezesha wakulima, wavuvi na wafugaji kuendesha shughuli
zao kwa tija kwa kuwapa elimu, zana na ushauri ili kukuza uchumi wa mkoa
kwa kuhusisha uwekezaji mdogo, wa kati na mkubwa lengo likiwa ni
kuongeza thamani ya mazao.
No comments:
Post a Comment