Thursday, 18 August 2016

AMUUA MKE NA YY KUJIUA GEITA

Mkazi wa Kijiji cha Kisabe kata ya Iparamasa, Sikujua Ally (21) anadaiwa kuuawa na mumewe, Elias Laurent (25) kwa kumchoma kisu tumboni kisha na yeye kujiua.

Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 12 saa 7.30 mchana baada ya mwanamke huyo kumtuhumu mumewe kutoka nje ya ndoa, jambo lililozusha hasira kwa Laurent na kumchoma kisu tumboni na kufa papo hapo.

No comments:

Post a Comment