Prof. leo kakomaa hataki kabisa kuambiwa amesimamishwa uanachama.
Hii safi sana maana maalim anaendesha chama kama mali yake.
Akihojiwa na mtangazaji Spencer Lamerk wa ITV usiku huu, Prof. Ibrahim
Haruna Lipumba amesema kuwa yeye bado ni Mwenyekiti halali wa CUF.
Prof. Lipumba amesema kuwa kufuatia kutengua barua yake ya kujiuzulu
Uenyekiti, aliandika barua kwa Katibu Mkuu wake kutaka kurejea kazini
kama Mwenyekiti. Katibu Mkuu alimjibu kuwa anatafuta ushauri wa
kisheria.
Kuhusu kikao cha Baraza Kuu la CUF kilichomsimamisha uanachama, Profesa
Lipumba amesema kuwa kikao hicho hakikuwa halali kwakuwa hakukuwa na
akidi ya Wajumbe wa kutoka Tanzania Bara. Amesema kuwa Katibu Mkuu
hamshirikishi Naibu Katibu Mkuu Bara na kuonekana akiendesha chama
kiimla.
Prof. Lipumba amesema kuwa Katibu Mkuu asipotaja tarehe ya yeye kurejea
kazini kama Mwenyekiti, atasubiri barua ya Msajili wa Vyama ili aanze
kazi tena kama Mwenyekiti wa taifa wa CUF.
No comments:
Post a Comment