Serikali ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha utaratibu wa
sheria,ya kuanzisha Bodi ya usajili wa walimu nchini, ambayo itasimamia
masuala yote ya walimu kitaaluma,uendelezaji na maadili ya kazi za
ualimu,na pia kudhibiti wimbi la walimu bandia nchini ambapo hivi sasa
kumezuka tabia ya watu kujiita walimu, na kuanzisha shule katika
mazingira yasiyofaa.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhandisi Stella
Manyanya, ameyasema hayo wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya walimu
wanaofundisha darasa la tatu na la nne,masomo ya Kiswahili, Kiingereza
na hisabati katika mikoa ya Rukwa na Katavi, na kwamba licha ya hatua
hizo kuboresha suala la utoaji wa elimu nchini,lakini pia Wizara
imepanga kuwabana maafisa udhibiti ubora wa elimu katika ngazi zote, ili
wasimamie walimu katika suala zima la ufundishaji.
Kwa upande wake Mratibu wa mafunzo wa wakala wa maendeleo ya uongozi wa
elimu Adem Bw Nyakeko Francis,amesema mafunzo hayo ambayo yamewagusa
zaidi ya walimu elfu moja kwenye mikoa ya Rukwa na Katavi, yanalenga
katika kusoma kuandika na kuhesabu, ili hatimaye asiwepo mtoto yeyote
anayemaliza shule ya msingi asiyejua kusoma na kuandika kama ilivyo hivi
sasa.
No comments:
Post a Comment