Thursday, 18 August 2016

AKUTWA AMEJINYONGA KWA SHUKA ASUBUHI YA LEO

Katika haliisiyo ya kawaida kijana mmoja ambaye jina lake halikufahamika amekutwa Asubuhi ya leo amejinyonga maeneo ya Mlimani City Opposite na Mawasiliano Tower.

Kwa mujibu wa Mashuhuda kijana huyu amekutwa amejinyonga na Kipande cha shuka na chini yake kulikuwa na begi lenye nguo yani inaonyesha kuwa huyu Kijana alikuwa katoka safarini pia marehemu amekutwa na anajiraha mkono wa Kushoto na damu katika flana maeneo ya kifuani.

Mashuhuda wanasema kuwa inawezekana kuwa huyu kijana alipigwa na watu kisha alipofariki wakamtundika Mtini ili aonekanike kama kajiyonyanga mwenyewe maana amekutwa kaumia mkononi pia ana damu kifuani kwamujibu wa mashuhuda wanasema mtu anayejinyonga huwa lazima akutwe kajinyea au kajikojolea marehemu amekutwa yuko safi kabisa, pia Mtu aliyejinyonga huwa atoki Damu kwaiyo inawezekana kuwa alipigwa kisha akatundikwa mtini ili aonekane kama kajinyonga mwenyewe..

M/mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.. Amin

No comments:

Post a Comment