Katika kuonyesha kuwa huu si wakati wa kudanganyana na kudhani kuwa kila Mtanzania ni " mbumbumbu
" hivyo kuwafanya unavyotaka jana Wananchi wa Rungwe Mkoani Mbeya
waliamua kumtandika Viboko Mwenyekiti wa Kijiji kwa kosa la kuwadanganya
kuhusu Mapato na Matumizi ya Kijiji chao kwa muda wa mwaka mzima.
Baada ya kuitisha huo Mkutano na Wanakijiji kuitikia kwa uwingi wao Mwenyekiti huyo alianza kuwasalimu kwa " mikogo " na " bashasha " zake nyingi kisha kuanza kuwasomea Wanavijiji hao mapato na matumizi ya Kijiji chao kwa mwaka mmoja.
Katika hali ya kushangaza kabisa na ambayo inasemekana ndiyo iliyoamsha
hasira na Wanavijiji huyo Mwenyekiti alisema kuwa kwa mwaka mzima Kijiji
chao kimekusanya Tsh 10,000/ tu huku akisisitiza Wanavijiji hao
kuendelea kuchangia kwa Maendeleo ya Kijiji chao.
Hapo ndipo Wanakijiji cha Rungwe walipoamua kumfundisha adabu huyo
Mwenyekiti wao na wakatumwa Watu baadhi kwenda porini kukata Fimbo
ambapo wakachaguliwa Watu watatu walioshiba kisawasawa kumtandika Viboko
huyo Mwenyekiti huku Wanavijiji wengine wakishangilia.
Mara baada ya kuchapwa hivyo Viboko Mwenyekiti huyo alisikika akisema nanukuu " asanteni
sana kwa kunichapa Viboko na nawaombeni mno radhi Ndugu zangu naahidi
kujirekebisha lakini hivi Viboko mlivyonichapa leo vitakuwa chachu
kwangu na Mimi pia kwenda kuwatandika Viboko hivi hivi tena zaidi
Watendaji wangu ambao kimsingi ndiyo wameniponza hadi leo nimeumbuka na
kuaibika hivi " mwisho wa kumnukuu Mwenyekiti aliyechapwa " bakora ".
Binafsi Kitendo hiki nimekipenda na kukifurahia mno kwani kinaonyesha
kuwa Wananchi wa sasa tena wale waishio Vijijini wanajitambua " kisawasawa " na kwamba wasichukuliwe " poa " labda kwakuwa hawajaenda Shule. Ningependekeza tu hiki Kitendo cha " Kishujaa
" cha Wanakijiji huko Rungwe kiigwe kwa nguvu zote na Watanzania
wengine sehemu mbalimbali za Kiutawala ili Watawala au wenye kupewa
dhamana ya kuwatumikia Wananchi wafanye Majukumu yao ipasavyo na kwa
kufanya hivyo nina amini Utendaji wa kiumakini utaonekana na maendeleo
ya haraka kupatikana.
Akhsanteni sana wana Rungwe.
No comments:
Post a Comment