Wasanii Orijino Komedi wahojiwa, washikiliwa polisi
Jeshi la Polisi Dar leo limewahoji wasanii wa Orijino Komedi makosa ya kuvaa sare za polisi kwenye harusi ya msanii mwenzao Emanuel Mgaya “Masanja”.
Wasanii hao, Lucas Muhuvile maarufu Joti, Alex John “Mac Reagan” na
Isaya Gideon “Wakuvanga” wamehojiwa leo sambamba na meneja wa kundi
hilo, Sekioni David.
Taarifa kutoka Jeshi la Polisi Dar zinaeleza
kuwa wasanii hao walikamatwa tangu jana jioni na kulala kituo cha Polisi
hadi walipohojiwa juu ya tukio hilo.
No comments:
Post a Comment