Saturday, 13 August 2016

MCHUNGAJI AENDA JELA MIAKA 20 KWAKUKUTWA NA MENO YA TEMBO

Mchungaji wa kanisa moja mkoa wa Katavi amehukumiwa kwenda jela miaka 20 mara baada ya kukutwa na meno ya tembo yapatayo vipande 100 ktk ofisi yake mwezi uliopita.

mchungaji huyo alikuta na vipande hivyo ndani ya ofisi mara baada ya rai wema kutoa taarifa kwa jesh la polisi mkoa wa Katavi na kumfuatilia na kukuta amevificha chini ya meza ndani ya gunia.

Hata hivyo mashahidi sita waliitwa kutoa ushahid huo mahakamani hapo jana mchana na kusema nikweli Mchungaji huyo alikutwa na vipande hivyo.

Akitoa hukumu hiyo hakim wa mkoa wa Katavi alisema ana muhukumu kwenda jela miaka 20 kwa kujishirikisha na makosa ya ujangili na kuhujum uchumi na kuuwa tembo pia kujihusisha na biashara ya meno ya tembo pasina kibali.

No comments:

Post a Comment