Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na jopo la
madaktari bingwa kutoka Misri, wakitumia dakika 90, jana walifanikisha
upasuaji wa kurekebisha tatizo katika njia ya mkojo kwa watoto pacha
waliokuwa wameungana Eliud na Elikana Mwakyusa (3) wakazi wa Kasumulu,
Kyela, Mbeya.
Katika upasuaji wa awali wa kuwatenganisha
uliofanyika India, watoto hao waliwekewa njia za dharura za mkojo lakini
jana wamewekewa za
kudumu.
No comments:
Post a Comment