Chama kikuu cha upinzani nchini Zambia kimepeleka kesi mahakamani
kupinga ushindi wa Rais Edgar Lungu uliofanyika mapema mwezi huu.
Mgombea wake wa urais Hakainde Hichelema, aliiambia BBC kuwa uchaguzi
huo uliibwa kutoka kwake na haukuonyesha matakwa ya watu wa nchi humo.
Chama chake cha National Development (UNDP) kimemuandikia spika wa
bunge, kikimtaka achukue wadhifa wa urais hadi uamuzi wa mahakama
utolewe.
Tume ya uchaguzi nchini Zambia ilikuwa imemtangaza Lungu kuwa mshindi
kwa asilimia 50.35 huku Hichilema akipata asilimia 47.67 na kusisitiza
kuwa uchaguzi ulikuwa wa haki.
Bwana Lungu alimshinda Hichilema uchaguzi uliotangulia mwaka uliopita kwa chini ya kura 28,000.
No comments:
Post a Comment