Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limebaini mbinu mpya za
wahalifu ya kuingiza bidhaa za magendo kwa kutumia ng’ombe.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam DCP Hezron Gymbi.
“Katika operesheni ya kuwasaka wahalifu sugu tumebaini watuhumiwa
wakibadili mbinu tofauti ya wizi wakitumia wanyama kama Punda na Ng’ombe
waliofundishwa kwa ajili ya kusafirisha bidhaa za magendo na kukwepa
kodi,” amesema.
Gymbi amesema kuwa wanyama hao huswagwa hadi katika ufukwe wa bahari na
kisha kuelekea kwenye boti inayoegeshwa katikati ya maji ambapo wanyama
hao hubebeshwa mizigo hadi walipo wahalifu.
“Kimsingi mbinu hizo tumeshabaini na tunazifanyia kazi,tunaendelea kuwasaka Wamiliki na wanyama hao,” amesema.
Amesema hivi karibuni alikamatwa Ng’ombe maeneo ya Mbweni katika ufukwe
wa bahari ya Hindi akiwa amebeba vitu mbalimbali zikiwemo TV, sukari na
sabuni ambavyo vyote havikulipiwa ushuru.
No comments:
Post a Comment