Serikali inatarajia kutoa ajira mpya zipatazo71,496 kwa mwaka huu wa
fedha baada ya kukamilika kwa zoezi la kuwaondoa wafanyakazi hewa ambapo
hadi sasa watumishi wapatao 839, tayari wapo katika hatua mbalimbali
wakiwepoo waliopelekwa katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU).
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,(Utumishi na Utawala Bora),Angela Kairuki
aliyasema hayo wakati akizungumzia juu ya utekelezaji na mikakati katika
Wizara yake katika kipindi cha “Utekelezaji” kinacho rushwa kupitia
Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC1).
“Mpaka sasa kuna baadhi ya watumishi hewa waliofanyiwa mahojiano na
polisi na kama upelelezi ukikamilika sheria kali zitachukuliwa ikiwepo
kufikishwa mahakani kwa mtumishi atakaye bainika kukutwa na makosa “
Alisema Kairuki
Alisema kuwa kuna baadhi ya Maofisa Utumishi pamoja na Wahasibu ambao
wameonekana kuwa si waaminifu kwani baadhi yao wameonekana kuelekeza
fedha kwa ndugu zao na miradi yao na wengine walishastaafu lakini majina
yao yameonekana bado kuendelea kuwepo katika mfumo wa kupokea.
Kairuki aliongeza kuwa katika kipindi cha Machi mosi mpaka kufikia
Agosti 20 mwaka huu, Watumishi hewa wapatao 16,127 walibainika ambapo
walikuwa wakisababishi hasara ya mabilioni kwa serikali ambapo serikali
kama ingewalipa ingesababisha hasara ya zaidi ya bilioni 16.
“Uhakiki huu ni endelevu kwani baadhi ya Maofisa Utumishi pamoja na
Wahasibu si waaminifu hivyo tunawataka waajiri wao kuweka mkazo katika
swala hili, kwani tunajua wahasibu wengi wamepewa madaraka lakini si
waamiifu”Alisema Kiruki.
Kairuki aliwatoa hofu baadhi ya Watanzani ambao walikuwa wakisubiria
ajira mpya kutoka Serikali, alisema kuwa kilichokuwa kikisubiriwa ni
takwimu halisi ambazo zitasaidia kuonesha ni watumishi wangapi wameweza
kuondolewa.
“hii ni neema kwa wanafunzi waliomaliza vyuo kwani kuna nafasi zipatazo
71,496 kwa mwaka huu wa fedha hivyo napenda kuwahauri vijana kuwa na
subira kwa kuto kujiingiza katika makundi yasiyo faa” Alisema kairuki.
Pia aliwataka Maofisa Utumishi kuwa hudumia vizuri watumishi kwa kuwapa
haki zao ikiwemo kuwa pandisha madaraja kwa wakati stahili na si vema
kwa baadhi ya watu kughushi taarifa za Utumishi wa umma na kusisitiza
kuwa kufanya hivyo ni kosa kuibwa sana.
No comments:
Post a Comment