ACT Wazalendo inataka kubadili miradi ya barabara za Ujiji? HAPANA.
Manispaa yetu ina Mradi wa tshs 9bn kujenga barabara na kujenga mfereji
wa Lubengela. Barabara inayojengwa ni 1.1km katika Mtaa wa Rusimbi,
Ujiji. Kwa mujibu wa mkataba barabara hii inajengwa kwa tshs 2.5bn ( ?
).
Hoja iliyopo mezani ni inawezekana vipi Manispaa yetu kujenga barabara Urefu huo kwa tshs 2.5bn?
TANROADS mkoa wa Kigoma imejenga barabara ya Bushabani katika Manispaa jumla ya 4km kwa tshs 1.7bn. Sisi tunawezaje kujenga 1.1km kwa tshs 2.5bn?
Hii ndio hoja tunayojadili na sio kubadili Mradi kuutoa Ujiji. Lengo
letu ni kujenga barabara nyingi zaidi za Lami kwa kutumia Fedha hiyo
hiyo. Kwa mfano barabara ya Shindika - Jihad - Kagashe inayounganisha
kata za Buzebazeba na Katubuka kuelekea Uwanja wa ndege na Barabara ya
Mwami Rusimbi, Gungu ni miongoni mwa barabara ambazo tungeweza
kutengeneza kwa pamoja na barabara ya Rusimbi.
Kuhuisha mji wa
Ujiji ni kipaumbele kikubwa sana cha ACT Wazalendo. Ndio maana tunajenga
Bandari Forodha ya Ujiji, tunajenga barabara ya Kasulu Road Ujiji,
tunajenga barabara ya pembezoni mwa ziwa kutoka Forodha ya Ujiji mpaka
Kikamba ( Bangwe ) na tunahimiza ujenzi wa barabara ya Bangwe - Ujiji
kupitia TANROADS.
Mimi binafsi nimezungumza na kukubaliana na
Waziri wa Elimu Ndg. Joyce Ndalichako kuhusu kuanzisha Chuo kikubwa cha
Ufundi Ujiji ( Ujiji Technical School ) kitakachokuwa na wanafunzi 5000.
Zaidi ya yote kuna Uwekezaji mkubwa kutoka kampuni moja kubwa
kutoka Shanghai, China kujenga na kuendesha Mradi wa Ujiji City ( trade
and logistic center ) ambao utajenga maduka 3000, nyumba za kisasa za
makazi na maghala ( warehouses). Lengo ni kuifanya Ujiji ni kituo cha
biashara katika eneo la Maziwa Makuu.
No comments:
Post a Comment