Mpaka
sasa michezo hiyo imekwishafanyika kwa kiwango kikubwa na hivyo kupata
Orodha ya timu zinazoongoza mpaka sasa katika kunyakuwa medali nyingi
kwa upande wa Dhahabu, Shaba pamoja na Fedha huku jumla ya mataifa 206
yanashiriki Olimpiki ya mwaka huu.
Marekani
ni nchi kinara katika medali hizo, huku ikiwa na jumla ya medali 22 kwa
kujumuisha michezo yote na mpaka kufikia sasa, akijinyakulia medali 6
za dhahabu, 8 za shaba pamoja na medali 8 za Fedha.
Nchi
inayofuatia ni China wakiwa na medali 16 mpaka sasa wakiwa na medali 7
za dhahabu medali 3 za shaba pamoja na medali 6 za fedha, kwa hiyo China
kuwa nchi ya kwanza kwa kuwa na medali nyingi za Dhahabu akifuatiwa na
Marekani ikifuatiwa na Australia.
Nchi
zingine ni pamoja na Australia mwenye medali 8 mpaka sasa huku akiwa na
medali 4 za dhahabu 4 za Fedha na kuambulia patupu katika medali ya
Shaba.
Kiujumla
katika medali zote Urusi imeshikilia nafasi ya nne kwa jumla ya medali
12, Japani 12 huku ikifuatiwa na Italia medali 9, Korea Kusini medali 6
pamoja na Ufaransa 6, Canad 5, huku Hungary pamoja na Thailand zikiwa na
medali 4.
Ujerumani
pamoja na Taipei ya China zote zina medali 3, huku wenyeji Brazil,
Ubelgiji, Ugiriki, Uholanzi, Sweden zote zikiwa na medali mbli kila
moja, na nchi pekee kutoka Afrika, Afrika Kusini ikiwa na jumla ya
medali mbili amabzo zote ni za Fedha moja ikipatikana katika kuogelea
walizoshinda Cameron Van De Burgh pamoja na Chad Le Clos
No comments:
Post a Comment