Tungeshangaa sana kama swali hili (kuhusu Prof. Lipumba kuhamia ACT)
lisingetokea kwa sababu na sisi kutwa nzima ya jana tumesikia hizo
fununu. Lakini naamini baada ya mkutano wetu huu na waandishi wa habari,
nyie waandishi mmethibitisha kuwa fununu hizo si za kweli. Chama chetu
sisi kipo wazi. Mtu yeyote ana haki ya kujiunga iwapo anakubaliana na
misingi, katiba na itikadi ya chama. Kwa hiyo mtu yeyote yule raia wa
Tanzania ambaye anajiona ni mzalendo ana uhuru wa kujiunga
na chama chetu. Pale ambapo jambo hilo litatokea tutawajulisha. Chama
chetu sisi ni cha uwazi. Kwa hiyo, tusingependa watu ambao wanatuwekea
maneno. Watu ambao wanatabiri vitu ambavyo kimsingi havipo kwa malengo
yao. Kwa mfano hizo fununu ambazo zilisambazwa jana zilikuwa fununu
zenye malengo hasi. Kwa sababu tunafahamu, wenzetu wa Chama cha Wanachi
CUF wana masuala yao yanayoendelea. Ni demokrasia ya ndani ya chama chao
ambayo sisi tusingependa kuiingilia. Sisi tungependa kuona wanamaliza
tofauti zao kwa amani ili kuimarisha mfumo wa vyama vingi katika nchi
yetu…Sisi tulikuwa na kikao cha kawaida kabisa cha chama (Kamati Kuu) na
tumejadili ajenda ambazo nimewaeleza (Hali ya nchi na masuala mengine
ya chama) na taarifa yetu tumeitoa na mmeiona. (Kwa hiyo) kama
nilivyoeleza hapo awali, mtu yoyote anayedhani kuwa anaweza kuendesha
siasa ndani ya Chama chetu, tunamkaribisha kwa mikono miwili na tutaweza
kufanya kazi kwa pamoja. Lengo letu sisi ni kuhakikisha mfumo wa vyama
vingi katika nchi yetu unaimarika. Lengo letu sisi ni kuifanya nchi yetu
iwe ya kidemokrasia na kuiondoa katika hali inayoendelea hivi sasa ya
kuwa kwenye utawala wa imla wa mtu mmoja ambaye yeye ndiye anayeamua
‘Kun faya kun’ linakuwa”
Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo.
Mkutano na waandishi wa habari, Tarehe 06 Septemba 2016
No comments:
Post a Comment