Thursday, 15 September 2016

APIGWA RISASI 3 KUKISIWA MWIZI KIMAKOSA

Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ni askari ambaye si yeye(bado haijathibitishwa kama ni mwanajeshi ama polisi) adaiwa kumpiga riasasi za miguuni mwanafunzi wa mwaka wa 2 katika chuo cha usimamizi wa fedha I.F.M kozi ya I.T (Information Tachnology) kilichopo jijini Dar es salaam akiwa hana silaha ya aina yoyote ile kwa kile kinachodaiwa kuwa kijana huyo kuitiwa kelele za mwizi na mlinzi wa nyumba ya jirani alipokuwa anapita akiwa anatoka kwenye birthday party akiwa peke yake maeneo ya Tabata chang'ombe.

Baada ya kuitwa mwizi kijana huyo alijisalimisha kwa mlinzi huyo wa nyumba ya jirani lakini mlinzi aliyeendelea kumpiga kijana kitendo kilichopelekea watu wengi kama 30 (akiwemo mtuhumiwa huyo) kujaa wa kitokea majumbani walipokuwa wamelala na kuanza kumpiga mwanafunzi huyo, ndipo ambapo mtuhumiwa huyo alitokea na kumimina risasi 3 tatu kwenye mguu wa kushoto na moja kwenye paja la mguu wa kulia.

Kijana huyo ajulikanaje kama Nicholas (miaka 25) mkazi wa Sinza, alipigwa risasi hizo, kisha mtuhuiwa kupiga simu katika kituo cha polisi Tabata ya kuwa wameua jambazi, kitendo kilichopelekea polisi hao kufika eneo la tukio na kukuta kuwa mwanafunzi huyo hakuwa jambazi hivyo polisi kumpakiza katika defender na kumpeleka hospitali ya taifa ya Muhimbili ambapo sasa anapata matibabu katika wodi ya Kibasila namba 13 akiwa hana pingu za polisi kwenye kitanda chake kama ambavyo jambazi anavyopaswa kufungwa

Na taarifa zilizopo ni kwamba cover-up ya nguvu ipo njiani kufanyika ili ionekana huyu mtuhumiwa alikuwa ameenda katika fumanizi la kimapenzi

Pole sana jirani yangu Mungu atakusaidia

Chanzo ni mimi mwenyewe ni mkazi wa Sinza na jirani yake

No comments:

Post a Comment