Kagera. Kampuni ya simu za mkononi, Tigo Tanzania imekabidhi madawati 235
yenye thamani ya Sh39 milioni kwa shule nane za msingi mkoani hapa ikiwa
ni kuunga mkono juhudi za serikali kumaliza uhaba huo.
Kupitia
kampeni ya Tigo Fiesta 2016, inatarajia kuinufaisha mikoa 18. Meneja wa
Tigo Kanda ya Ziwa, Edgar Mapande, alisema uhaba wa madawati ni moja ya
sababu zinazoathiri uwezo wa kujifunza na kupunguza ufanisi wa wanafunzi
.
No comments:
Post a Comment