Shirika la Maji Safi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO) limetangaza
kuzima mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Juu kwa wakazi wa Dar es salaam
na Mji wa Kibaha Pwani kwa saa 14 kesho Ijumaa kuanzia saa tatu asubuhi
mpaka saa tano usiku.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa kwa
vyombo vya Habari na ofisi ya mahusiano ya shirika hilo leo jijini Dar
es Salaam inaeleza kuwa sababu kuu ya kuzimwa kwa mtambo huo ni
kuruhusu usafishaji wa bomba jipya na kufanya majaribio ya sehemu ya
mtambo mpya wa Maji wa Ruvu juu.
No comments:
Post a Comment