Tuesday, 6 September 2016

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI KESI DHIDI YA LUNGU

Mahakama ya Kikatiba nchini Zambia imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na mgombea wa urais wa chama cha upinzani cha United Party for National Development (UPND), Hakainde Hichilema kupinga ushindi wa Rais Edgar Lungu.
Katika kesi hiyo Hichilema alikuwa ameshirikiana na mgombea wake mwenza waliodai kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilikuwa imechakachua matokeo kwa lengo la kumpendelea mgombea wa chama tawala.

No comments:

Post a Comment