Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ni askari ambaye si yeye(bado
haijathibitishwa kama ni mwanajeshi ama polisi) adaiwa kumpiga riasasi
za miguuni mwanafunzi wa mwaka wa 2 katika chuo cha usimamizi wa fedha
I.F.M kozi ya I.T (Information Tachnology) kilichopo jijini Dar es
salaam akiwa hana silaha ya aina yoyote ile kwa kile kinachodaiwa
kuwa kijana huyo kuitiwa kelele za mwizi na mlinzi wa nyumba ya jirani
alipokuwa anapita akiwa anatoka kwenye birthday party akiwa peke yake
maeneo ya Tabata chang'ombe.
Baada ya kuitwa mwizi kijana huyo alijisalimisha kwa mlinzi huyo wa
nyumba ya jirani lakini mlinzi aliyeendelea kumpiga kijana kitendo
kilichopelekea watu wengi kama 30 (akiwemo mtuhumiwa huyo) kujaa
wa kitokea majumbani walipokuwa wamelala na kuanza kumpiga mwanafunzi
huyo, ndipo ambapo mtuhumiwa huyo alitokea na kumimina risasi 3 tatu
kwenye mguu wa kushoto na moja kwenye paja la mguu wa kulia.
Kijana huyo ajulikanaje kama Nicholas (miaka 25) mkazi wa Sinza,
alipigwa risasi hizo, kisha mtuhuiwa kupiga simu katika kituo cha polisi
Tabata ya kuwa wameua jambazi, kitendo kilichopelekea polisi hao kufika
eneo la tukio na kukuta kuwa mwanafunzi huyo hakuwa jambazi hivyo
polisi kumpakiza katika defender na kumpeleka hospitali ya taifa ya Muhimbili
ambapo sasa anapata matibabu katika wodi ya Kibasila namba 13 akiwa
hana pingu za polisi kwenye kitanda chake kama ambavyo jambazi
anavyopaswa kufungwa
Na taarifa zilizopo ni kwamba cover-up ya nguvu ipo njiani kufanyika
ili ionekana huyu mtuhumiwa alikuwa ameenda katika fumanizi la kimapenzi
Pole sana jirani yangu Mungu atakusaidia
Chanzo ni mimi mwenyewe ni mkazi wa Sinza na jirani yake
No comments:
Post a Comment