Mwanzilishi
wa kampuni ya Facebook Mark Zuckerberg amelezea kusikitishwa kwake
baada ya satelaiti ambayo Facebook ingeitumia kwa mawasiliano ya kasi ya
mtandao wa intaneti barani Afrika kuharibiwa.
Satelaiti hiyo iliharibiwa katika mlipuko uliotokea eneo la Cape Canaveral jimbo la Florida, Marekani siku ya Alhamisi.
Satelaiti hiyo kwa jina Amos-Six ilikuwa imebebwa na roketi ya Falcon
Nine ambayo ililipuka ilipokuwa ikifanyiwa majaribio ya kujiandaa kwa
safari ya siku ya Jumamosi.
Mlipuko huo ulitokea wakati roketi hiyo ilikuwa ikijazwa mafuta na kutikiza majengo yaliyokuwa umbali wa kilomita kadha.
Bw Zuckerberg, ambaye yumo ziarani Afrika, amesema "nimesikitishwa sana" kusikia kwamba satelaiti hiyo iliharibiwa.
"Tutaendelea kujitolea katika lengo lengo la kufikisha huduma ya mtandao
kwa kila mtu na tutatia bidii hadi kila mtu apate nafasi na manufaa
ambayo yangetokana na satelaiti hii," aliandika kwenye ukurasa wake wa
Facebook.
Hakuna aliyejeruhiwa wakati wa mkasa huo.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa kulipuka kwa roketi hiyo ni pigo kubwa kwa
mwanabiashara Elon Musk ambaye ni mmiliki wa kampuni ya kuunda roketi
ya Space X.
Afisa mmoja wa masuala ya anga za juu wa Israeli amesema satelaiti ya
Amos-6 inakadiriwa kuwa na thamani ya $200m (£150m) na ilimilikiwa na
kampuni kwa jina Spacecom, was a major blow to the industry.
"Hili ni pigo kubwa sana ambalo huenda ikaathiri mustakabali wa sekta ya
satelaiti na huenda ikahitaji kupigwa jeki (kifedha)," alisema
mwenyekiti wa taasisi ya masuala ya anga za juu ya Israel, Isaac
Ben-Israel.
No comments:
Post a Comment