MAGUFULI ATISHIA KUBADILI NOTI KUWABANA WANAOFICHA FEDHA
Katika kile kinachoonekana kutaka kuwadhibiti watu wanaodaiwa kuficha
fedha, Rais John Magufuli amesema kwa mamlaka aliyonayo anaweza kuamua
kubadili fedha ili zile zinazofichwa na watu hao wakose mahali pa
kuzipeleka.
Akizungumza katika mkutano wa 14 wa mwaka wa
wahandisi uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City leo mchana mjini
hapa, Magufuli amesisitiza kuwa kauli hiyo ni mahsusi kwa watu
walioficha fedha katika majumba yao na kuwataka kuachana na tabia hiyo
mara moja ili fedha hizo ziingie katika mzunguko.
No comments:
Post a Comment