Thursday, 1 September 2016

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA AMLIMA KALI BARUA MAALIM SEIF

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa imemuandikia barua Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif kufuatia Prof. Lipumba kupeleka malalamiko kuwa hakutendewa haki na kikao anachokita kikao batili cha chama chao.

Ikumbukwe 17.8.2015 Prof. Lipumba alijiuzuru nafasi yake ya Uenyekiti wa Chama na kubaki wazi takribani mwaka mmoja na siku kadhaa na yy kuwa kama mwanachama wa kawaida ktk chama hicho.

Zikiwa zimebakia siku chache kabla ya kutimiza mwaka Prof. Lipumba aliandika barua ya kutengua uamuzi wake wa kujivua uenyekiti wa chama hicho huku chama cha CUF kikiwa hakina mwenyekiti wala kufanya kikao cha kamati kuu kupitia barua ya Prof. Lipumba.

No comments:

Post a Comment