Friday, 9 September 2016

VIFUNGU VILIVYO VIMEVUNJWA NA BARAZA KUU KUFUATIA MAAZIMIO YAO HUKO ZANZIBAR

VIFUNGU HIVI VITANO VIMEVUNJWA NA BARAZA KUU KUFUATIA MAAZIMIO YAO HUKO ZANZIBAR
1. 81 (4) . "maamuzi muhimu yatahesabiwa kuwa halali ikiwa zaidi ya theluthi mbili ya wajumbe kutoka Tanzania bara na zaidi ya theluthi mbili ya wajumbe kutoka Tanzania Zanzibar watayaunga mkono" 81 (4) ikatoa ufafanuzi nanukuu hapa kuhusu maamuzi muhimu " kwa madhumuni ya kijifungu cha (4) cha kifungu hiki maamuzi muhimu yatahusu mambo yote yaliyoorodheshwa katika kifungu cha 77 (8) cha katiba hii na kama yatakavyorekebishwa Mara kwa Mara "kifungu chenyewe 77(8) nakinukuu hapa " kwa madhumuni ya kifungu cha 7 cha kifungu hiki maamuzi muhimu ni pamoja na ...........(d) kuwasimamisha, kuwaachisha , au kuwafukuza uongozi na /au uanachama viongozi wakuu wa kitaifa wa chama pamoja na viongozi wengine wa kitaifa kama ilivyoainishwa katika katiba hii. "
HIKI NI MOJA YA KIFUNGU KILICHOVUNJWA NA BARAZA KUU NA BADO NITAWEKA VIFUNGU VINGINE VINNE , HOJA YANGU HAPA NI NINI ?!
Ukichukua akidi iliyotangazwa na idadi ya wajumbe kutoka bara ambao hawakwenda znz katika kikao hicho cha baraza unashangaa maamuzi haya yalifikiwajwe ? ninao ushahidi wajumbe 14 kutoka bara hawakuja znz hivyo akidi ya 2\3 ya wajumbe kutoka bara haikutimia , hivyo maamuzi hayo kukosa uhalali wa kikatiba na kuwa violations kubwa ya katiba ya 1992 ya CUF -Chama cha wananchi, toleo la 2014

KWA TAARIFA YAKO JUA HILI...
 wajumbe wote kwa taarifa ya mheshimiwa mazrui ni 60, waliohudhuria na kupitisha maamuzi kwa kauli moja (unanimously) ni 46, wajumbe 14 kutoka bara hawakwenda na wajumbe wote kutoka bara ni 32 , tafuta 2\3 ya 32 utapata 21, na wajumbe wote wa znz walikuwepo ! 46 - 28 = 18 ni dhahiri akidi kutoka bara haikutimia wala kuzingatiwa ndio maana maamuzi yalikuwa kwa kauli moja

WAJUMBE AMBAO HAWAKUUDHURIA NA MAJINA YAO NI HAWA NDIO WANATENGUA VIFUNGU VYA KATIBA YA CUF
 
1. Magdalena sakaya 2. abdul kambaya 3. masoud omary 4. kapasha kapasha 5. thomas malima 6. nuru bafadhili 7. julius sa!amba 8. karume mgunda 9. zainabu mkiwa 10. Moza abeid 11. shabani kaswaka 12. ashura mustafa 13. fatuma chitepet na 14. athumani henku , hawa wote kutoka bara hawakuhudhuria

JIULIZE JE PROF. LIPUMBA KATENDEWA HAKI AU LAA MIMI SIJUI.

No comments:

Post a Comment