Wednesday, 7 September 2016

MH. FREEMAN MBOWE AANZA MOTO WAKE BUNGENI SASA


Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni amehoji deni la taifa na kukua na kuzidi shilingi trilioni 51 ambayo ni karibia mara mbili ya bajeti ya taifa, amesema kukopa ni muhimu lakini ni vyema kukawa na kiwango cha kudhibiti ukopaji ili taifa liondokane na mzigo wa riba na fedha zake zitumike kwenye miradi ya maendeleo na sio kulipa riba.

Ameuliza pia kuhusu Tanzania ilikuwa imesamehewa madeni yake na kufiia chini ya dola bilioni 10 kwa sababu ilikuwa kwenye nchi za HIPC (Heavily Indebted Poor Coutries), ni kwa nini serikali isifanye iniatiative ya kurudishshwa wenye mpango wa HIPC ili wasamehewe madeni na fedha za kulipa madeni zitumike kwenye kuleta maendeleo
Deni la taifa limeongezeka kwa asilimia 18 tangu JPM aingie madarakani (miezi 10 tu).

Akijibu swali hilo Naibu waziri wa fedha amesema serikali haijaondoka katika mpango huo lakini kuna nchi za Iran na Iraq amabzo zilikuwa zinafanya mchakato ili Tanzania isamehewe madeni yake lakini zilisitisha kutokana na migogoro ya nchi hizo

Naye Mwigulu Nchemba amesema fedha zinazokopwa zinatumiwa kufanya miradi ya maendeleo na nchi zinakopeshwa kulingana na uwezo wake wa ku service deni lake, na serikali haikopi kwa ajili ya matumizi ya kawaida bali kufanya miradi ya maendeleo ambayo itarudisha deni hilo

No comments:

Post a Comment