Imebainika kwamba mgogoro unaoendelea kufukuta ndani ya CUF unabebwa
zaidi na hoja dhidi ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa baada ya
aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba kuendelea
kutumia jina hilo kama sababu za mvurugano unaokikabili kwa sasa.
Katika mahojiano na kituo cha redio cha Clouds FM, Profesa Lipumba
amesema mkutano wa chama hicho uliomridhia Lowassa kuingia Ukawa
ulifanyika Zanzibar bila yeye kuambiwa, kitendo kinachoonyesha kuwa
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad alikuwa akimzunguka.
No comments:
Post a Comment