Thursday, 8 September 2016

MSWADA WA MABADILIKO KTK MIFUKO YA JAMII


Mswada wa mabadiliko ya sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii uko tayari. Fao la kujitoa halipo kwenye mapendekezo hayo, badala yake limeletwa fao la kutokua na ajira

Inapendekezwa kuwa, mfanyakazi ambaye amechangia zaidi ya miezi 18 atalipwa 30% ya mshahara wake wa mwisho baada ya kupoteza ajira. Na atalipwa kwa miezi 6 mfululuzo, baaada ya hapo malipo hayo yatasitishwa.

Mfanyakazi anayestahili malipo haya, ni yule tu ambaye hakuacha kazi kwa hiari yake (resignation)

Baada ya miaka 3 tangu kusitishwa kwa fao la kujitoa, mfanyakazi atakayekuwa hajapata ajira ataruhusiwa kuhamisha michango yake kutoka kwenye mfuko wa lazima (compulsory scheme), kwenda mfuko wa hiari (supplementary scheme). Hapo atakuwa na hiari kuchukua pesa yake kulingana na mfuko wa hiari aliojiunga nao na pia atakuwa na haki ya kuendelea kuchangia.

Mfanyakazi aliyeachishwa kazi akiwa amechangia chini ya miezi 18, atakuwa na haki ya kuchukua 50% ya michango yake mara baada ya ajira kukoma.

Hapa ndio wafanyakazi na vyama vya wafanyakazi tunatakiwa tuunganishe nguvu kutetea maslahi ya wafanyakazi ambao hawana ajira za kudumu.

No comments:

Post a Comment