Wednesday, 12 October 2016
VIGOGO 1500 HAWATAFIKA KTK MAADHIMISHO YA KUUZIMA MWENGE SIMIU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli ameagiza viongozi wote wa Serikali walioalikwa kuhudhuria sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa zitakazofanyika tarehe 14 Oktoba, 2016 katika Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu kutohudhuria sherehe hizo na wale ambao walishalipwa fedha ya posho na safari kwa ajili hiyo wazirejeshe
Taarifa iliyotolewa leo tarehe 12 Oktoba, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais Magufuli ametoa maagizo hayo ikiwa ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kubana matumizi yasiyo ya lazima na kuelekeza rasilimali nyingi katika shughuli za maendeleo ya nchi.
Waliozuiwa na wakuu wa Mkoa, Wilaya, Wakurugenzi wate wa Miji, Majiji na Manispaa wengine ni Wenyeviti wa Halmashauri na Mameya wa Miji na Majiji pamoja na Madereva wao na Watumishi wote wanao ambatanao kila mwaka.
Mgeni rasmi katika shughuli hiyo atakuwa n Rais wa Zanzibar a mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Zanzibar Mh. Dkt Ali Mohamed Sheni
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment