Wednesday, 12 October 2016

MIGOGORO, UNAFIKI WA VIONGOZI VINAUA VYAMA VYA SIASA NCHINI




Moja ya viashiria vya demokrasia katika nchi yoyote ni kuwa na vyama vya siasa ambavyo vinatimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria za nchi na katiba zao walizojiwekea. Msingi mkuu wa demokrasia ya vyama vingi ni Katiba ya nchi.

Nchi yetu iliruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, na hapo tukashuhudia kuanzishwa kwa vyama mbalimbali vya siasa. Mpaka sasa Tanzania ina vyama vya siasa 22 vyenye usajili wa kudumu.

Hata hivyo, vyama vingi ni dhaifu na vinashindwa kutoa ushindani kwa chama tawala (CCM). Udhaifu huo unasababishwa na ubinafsi wa viongozi ambao unasababisha migogoro ndani ya vyama hivyo.

No comments:

Post a Comment