Katika mambo ya msingi ambayo Chama cha ACT-Wazalendo kinapaswa kupongezwa ni hatua yake ya kuibua upya vuguvugu la Katiba Mpya, hii ndiyo ajenda muhimu kwa upinzani sasa.
Nathubutu kusema hii ni kete muhimu ambayo nilifikiri baada ya Rais John Magufuli kuingia madarakani, Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na vyama vya upinzani vingeibeba kama ajenda.
Hii ni kutokana na ukweli kuwa karibu ajenda zote za upinzani walizojinadi nazo wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka jana, kwa sehemu kubwa zimebebwa na zinatekelezwa na Rais Magufuli
No comments:
Post a Comment