Afisa
wa cheo cha juu serikalini ameiambia BBC kwamba wasichana 21 waliokuwa
miongoni mwa wasichana wa shule waliotekwa na wapiganaji wa Boko Haram
eneo la Chibok sasa wako huru.
Taarifa zinasema wasichana hao kwa sasa wamo mikononi mwa maafisa wa
usalama katika mji wa Maiduguri, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Msemaji wa Rais Muhammadu Buhari amethibitisha kuachiliwa huru kwa wasichana hao.
Bw Mallam Garba Shehu ameandika kwenye Twitter: "Imethibitishwa kwamba
wasichana 21 wa Chibok wameachiliwa na kwa sasa wamo mikononi mwa Idara
ya Masuala ya Serikali."
Haijabainika iwapo wasichana hao walikomombolewa na wanajeshi au waliachiliwa huru na wanamgambo hao.
Jeshi la Nigeria kwa muda limekuwa likiendesha operesheni kubwa ya kijeshi katika msitu wa Sambisa, ngome ya Boko Haram.
Wapiganaji wa kundi hilo waliteka wasichana takriban 250 waliokuwa wakilala kwenye mabweni shuleni Aprili mwaka 2014.
Kisa hicho kilishutumiwa vikali na jamii ya kimataifa.
Tangu wakati huo, ni msichana mmoja pekee aliyekuwa ameokolewa.
Kundi la kujihami la wanakijiji lilimpata Amina Ali Nkeki mwezi Mei
akiwa na mumewe, ambaye anatuhumiwa kuwa mwanachama wa Boko Haram,
pamoja na mtoto wake.
No comments:
Post a Comment