Monday, 17 October 2016
WAFANYAKAZI TBS, TRA WAKALIA KUTI KAVU
Serikali imewataka baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) walioshirikiana na wenzao wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupitisha makontena zaidi ya 100 bila kukaguliwa na shirika hilo katika Bandari ya Dar es Salaam kujisalimisha haraka.
HATIMA YA UBUNGE WA LONGIDO KUJULIKANA WIKI HII
Hatima ya ubunge katika Jimbo la Longido mkoani Arusha, inatarajiwa kujulikana wiki hii baada ya jopo la majaji wanaosikiliza rufaa iliyowasilishwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Onesmo Ole Nangole kutolewa uamuzi.
http://www.mwananchi.co.tz/…/1597578-3419528-us1…/index.html
Friday, 14 October 2016
40+ Employment Opportunities today 14 October, 2016
The Elizabeth
Glaser Pediatric AIDS Foundation is a global leader in the fight against
pediatric HIV and AIDS, working in 16 countries and at over 7,000 sites
around the world to prevent the transmission of HIV to children, and to
help those already infected. Today, because of the highly successful
work of the Foundation and its partners, pediatric AIDS has been
virtually eliminated in the United States. With a growing global staff
of over 1,000—nine of 10 who work in the field—the Foundation’s global
mission is to implement prevention, care, and treatment; further advance
innovative research; and to execute strategic and targeted global
advocacy activities to bring dramatic change to the lives of millions of
women, children, and families worldwide.
The Elizabeth
Glaser Pediatric AIDS Foundation Tanzania was recently awarded
Comprehensive Health Service Delivery Award by USAID which focuses on
comprehensive health services delivery for preventive and curative
services for FP, HIV/AIDS and TB.
As a result we are looking for passionate new members to join our team in the following positions.
For detailed Job descriptions and to apply visit correspondence link.
Associate Director of Project Implementation
Associate Director of Strategic Information and Evaluation
Associate Manager Health Information Systems
Associate Project Manager
Council Project Coordinator
Data Analyst/Biostatistician
Evaluation Officer
Project Grants Coordinator
Grants Officer
Health Information Systems Officer
Health Information Systems Officer
Informatics Officer
Project Driver (7 Posts)
Project Compliance Officer
Project Finance & Operations Manager
Project Financial Analyst
Project Officer for Adolescent and Youth Service
Project Officer Community Engagement
Project Officer Laboratory Services
Project Operations Assistant
Project Logistics Coordinator
Quality Improvement Manager
Quality Improvement Officer
Senior Manager Community Engagement
Senior Manager Evaluation
Senior Manager Health Information Systems
Senior Project Manager
Technical Specialist TB Services
Source: The Guardian 13 October, 2016 ============
MKE WA RAIS ATOA ONYO KALI HUKO NIGERIA
Mke
wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, ameonya kuwa huenda asimuunge
mkono mumewe kwenye uchaguzi mkuu ujao iwapo kiongozi huyo hatafanya
mabadiliko kwenye serikali yake.
Kwenye mahojiano na BBC, Aisha Buhari amesema rais huyo "hawafahamu" wengi wa maafisa wakuu aliowateua serikalini.
Amedokeza kwamba serikali imetekwa, na kwamba kuna "watu wachache" ambao huamua ni nani watateuliwa au kupewa kazi na rais.
Bw Buhari alichaguliwa mwaka jana baada yake kuahidi kukabiliana na ufisadi uliokuwa umekithiri serikali pamoja na ubaguzi na mapendeleo.
Uamuzi wa mke wa kiongozi huyo kusema hayo hadharani umeshangaza wengi, lakini ni ishara ya kiwango cha kutoridhishwa kwa watu na uongozi wa Rais Buhari, anasema mwandishi wa BBC aliyepo Abuja, Naziru Mikailu.
Rais Buhari alitangaza wakati wa kuapishwa kwake kwamba yeye "hamilikiwi na mtu yeyote na anamilikiwa na watu wote".
Kwenye mahojiano na Naziru Mikailu, Bi Buhari alisema: "Rais hawafahamu 45 kati ya 50, kwa mfano, kati ya watu aliowateua na mimi mwenyewe siwafahamu, licha ya kwamba nimekuwa mke wake kwa miaka 27."
Amesema watu ambao hana maono sawa na ya chama tawala cha All Progressives Congress (APC) sasa wanateuliwa kwenye nyadhifa kuu kwa sababu ya ushawishi wa "watu wachache".
"Watu wengine wanaketi manyumbani mwao wakiwa wametulia kisha wanaitwa na kupewa kazi ya kuongoza idara au kuwa mawaziri."
Aliopulizwa awataje watu waliokuwa wameteka serikali, alikataa na kusema: "Utawajua ukitazama televisheni".
Kuhusu iwapo Rais bado anadhibiti serikali, alisema: "Hilo ni watu wataamua."
Bi Buhari alisema mumewe bado hajamwambia iwapo atawania urais uchaguzi wa mwaka 2019.
"Bado hajaniambia lakini nimeamua, kama mkewe, kwamba mambo yakiendelea hivi hadi 2019, sitatoka kwenda kumsaidia kwenye kampeni na kuomba wanawake wampigie kura kama nilivyofanya awali. Sitafanya hilo tena."
Alipoulizwa ni jambo gani anachukulia kuwa ufanisi mkubwa wa serikali, alisema ni kuimarisha usalama kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ambapo serikali imekuwa ikikabiliana na wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram ambao walianza maasi 2009.
"Hakuna anayelalamika kuhusu kushambuliwa nyumbani kwake. Twashukuru kwamba sasa watu wanaweza kutembea bila kusumbuliwa, na kwenda maeneo ya ibada na kadhalika. Hata watoto Maiduguri wamerejea shuleni," Bi Buhari alisema, akirejerea mji huo ambao wakati mmoja ulikuwa makao makuu ya Boko Haram.
Chanzo: BBC

KUMBUKUMBU YA MWALIM N GUMZO LA JIJI NANI WA KUFANANISHA NAE?
Kumbukumbu ya miaka 17 ya kifo cha Mwasisi wa Taifa la Tanzania
Mwl.Julius Nyerere na wiki ya vijana , inaenda sambamba na uzimwaji wa
Mwenge wa uhuru Mkoani Simiyu, ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Zanzibar
Dkt.Ali Mohamed Shein Mkoani Simiyu.
TATIZO LA MACHO NI KUBWA SANA HAPA NCHINI
Asilimia 80 ya watanzania wana matatizo mbalimbali ya macho ambayo
wakati mwingine yanasababisha upofu huku serikali ikitakiwa kutoa elimu
ya namna ya kujikinga na tatizo hilo.
Serikali imeombwa kusogeza huduma za macho katika hospitali za wilaya pamoja na vituo vya afya ili kuwasaidia wagonjwa wenye matatizo ya macho kwa lengo la kuwasaidia watu wenye matatizo ya macho wakiwemo wale wenye matatizo ya kisukari .

Thursday, 13 October 2016
21 WAACHIWA NA BOKO HARAM NIGERIA
Afisa
wa cheo cha juu serikalini ameiambia BBC kwamba wasichana 21 waliokuwa
miongoni mwa wasichana wa shule waliotekwa na wapiganaji wa Boko Haram
eneo la Chibok sasa wako huru.
Taarifa zinasema wasichana hao kwa sasa wamo mikononi mwa maafisa wa usalama katika mji wa Maiduguri, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Msemaji wa Rais Muhammadu Buhari amethibitisha kuachiliwa huru kwa wasichana hao.
Bw Mallam Garba Shehu ameandika kwenye Twitter: "Imethibitishwa kwamba wasichana 21 wa Chibok wameachiliwa na kwa sasa wamo mikononi mwa Idara ya Masuala ya Serikali."
Haijabainika iwapo wasichana hao walikomombolewa na wanajeshi au waliachiliwa huru na wanamgambo hao.
Jeshi la Nigeria kwa muda limekuwa likiendesha operesheni kubwa ya kijeshi katika msitu wa Sambisa, ngome ya Boko Haram.
Wapiganaji wa kundi hilo waliteka wasichana takriban 250 waliokuwa wakilala kwenye mabweni shuleni Aprili mwaka 2014.
Kisa hicho kilishutumiwa vikali na jamii ya kimataifa.
Tangu wakati huo, ni msichana mmoja pekee aliyekuwa ameokolewa.
Kundi la kujihami la wanakijiji lilimpata Amina Ali Nkeki mwezi Mei akiwa na mumewe, ambaye anatuhumiwa kuwa mwanachama wa Boko Haram, pamoja na mtoto wake.

Subscribe to:
Posts (Atom)